NGULI wa soka wa Brazil, Roberto Carlos amemponda mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto’o akidai kuwa nyota huyo wa zamani wa klabu ya Anzhi Makhachkala siku zote hujiweka yeye mbele kuliko timu. Carlos na Eto’o mara ya kwanza walicheza pamoja katika klabu ya Real Madrid kwenye miaka ya 90 kabla ya kuungana tena Anzhi mwaka 2011 lakini Carlos ambaye kwasasa ni kocha msaidizi wa klabu hiyo ameonyeshwa kutofurahishwa na tabia alizokuwa akionyesha Eto’o wakati akiwa huko. Carlos amesema amemfahamu Eto’o toka akiwa na umri wa miaka 16 na amekuwa akimpenda kwasababu ni mtu mwema lakini siku zote amekuwa akijifikiria mwenyewe tu na sio wengine. Beki huo wa zamani alidai ameshindwa kumuelewa Eto’o kwani katika kipindi chote alichokuwa naye Anzhi yeye amekuwa akiwaleta wachezaji ambao ni marafiki zake na kutaka kuingilia kazi za watu. Carlos alifika mbali zaidi na kudai kuna wakati Eto’o alitaka kuiendesha klabu anavyotaka yeye kwa kuchukua nafasi yake pamoja na kocha Guus Hiddink.
No comments:
Post a Comment