Wednesday, September 25, 2013

LEWANDOWSKI KUJIUNGA NA BAYERN JANUARI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Robert Lewandowski amebainisha kuwa atajiunga na Bayern Munich katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani na kumaliza utata juu ya mustakabali wake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa akihusishwa na tetesi za kuhama Dortmund katika usajili wa majira ya kiangazi lakini klabu hiyo ilimkatalia kuondoka na kumlazimisha kucheza kwa msimu mwingine. Akihojiwa Lewandowski alithibitisha nia yake ya kwenda Munich na kwamba anatarajia kusaini mkataba Januari utakamuwezesha kujiunga na wababe hao wa soka nchini Ujerumani. Nyota huyo wa kimataifa wa Poland amefunga mabao 80 katika mechi 149 alizoichezea Dortmund toka ajiunge nao akitokea Lech Poznan mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment