Wednesday, September 25, 2013

MESSI AKASIRISHWA NA TAARIFA ZA UONGO DHIDI YAKE.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amejibu kwa hasira taarifa kwamba alionyesha ishara baada ya kutolewa katika mchezo dhidi ya Real Sociedad ambao ulichezwa jana na Barcelona kuibuka na ushindi wa mabao 4-1. Katika mchezo huo Messi mwenye umri wa miaka 26 alifunga bao lake la saba msimu huu lakini kocha Gerard Martino alimtoa nje zikiwa zimebakia dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika. Vyombo vya habari vya Hispania viliripoti kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina hakufurahishwa na hatua ya Martino kumtoa nje. Akijibu tuhuma hizo Messi amekanusha kuonyesha ishara yoyote wakati akitoka na kudai kuwa hawezi kuvumilia uongo unaotolewa na vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment