Thursday, September 26, 2013

WAZIRI TUNISIA AOMBA FIFA KUVUNJA SHIRIKISHO LA NCHI HIYO.

WAZIRI wa michezo wa Tunisia, Tarak Dhiab ametuma barua rasmi kwa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutengua uongozi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo na kuzua msuguano mkubwa kati ya shirikisho hilo na wizara. Taarifa hizo zilipokelewa kwa mshangao mkubwa na wadau wa soka wa nchi hiyo ambapo hakuna sababu yoyote iliyotolewa na waziri kwa madai yake aliyoomba FIFA. Shirikisho hilo linatarajiwa kukutana katika mkutano wa dharura utakaohudhuriwa na wajumbe wa kamati ya utendaji na wawakilishi kutoka wizara hiyo ili kujadili kinachoweza kutokea kutokana na maombi ya Dhiad. FIFA haijatoa taarifa yoyote kuhusiana na hilo, hata hivyo msemaji wa shirikisho hilo Nabil Dabboussi amesema hatua hiyo ya waziri inaweza kupelekea vilabu vya Tunisia vikafungiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika pamoja na ile ya Kombe la Shirikisho.

No comments:

Post a Comment