Monday, September 23, 2013

MADRID KUMKOSA BALE JUMATANO.

KLABU ya Real Madrid imethibitisha kuwa winga wake mahiri Gareth Bale amepata maumivu ya paja hivyo kuwa na hatihati ya kukosekana katika mchezo wa Jumatano dhidi timu ya Elche. Bale alitarajiwa kuwemo katika kikosi cha Madrid kwenye mchezo dhidi ya Getafe Jana lakini aliondolewa baada ya kupata majeraha hayo wakati wakipasha misuli moto kabla ya mechi. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imedai kuwa vipimo alivyofanyiwa Jumatatu asubuhi vimegundua tatizo hilo ambalo linaweza kumuweka nje ya uwanja kwa siku kadhaa. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Ancelotti amesema Bale anatarajiwa kuwa fiti katika mechi ya Jumamosi ijayo dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid, ingawa hata hivyo hakuwa na uhakika wa nafasi yake kwenye mechi ya katikati ya wiki.

No comments:

Post a Comment