Monday, September 23, 2013

SARE YAMSONONESHA BLANC.

MENEJA wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Laurent Blanc ameeleza kusikitishwa kwake na matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Monaco jana na kudai kuwa kikosi chake kilihitaji matokeo mazuri zaidi ya hayo. Bao la mapema lilifungwa na Zlatan Ibrahimovic liliipa uongozi wa mapema PSG kwenye mchezo huo lakini mshambuliaji nyota wa Monaco Radamel Falcao alisawazisha bao hilo dakika 20 baadae na kupelekea timu hizo kugawana alama. Blanc amesema pamoja na kwamba Monaco walicheza vyema lakini kama na wao wangetumia vyema nafasi nyingi za wazi walizopata hakuna shaka kwamba wangeibuka kidedea kwenye mchezo huo. Kocha amesema inabidi wachezaji wachezaji wake wafanyie kazi suala hilo kwani kama wanatengeneza nafasi nyingi halafu wanakuwa hawazitumii sio rahisi kupata matokeo wanayohitaji. PSG inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 wakiwa nyuma Monaco kwa alama mbili.

No comments:

Post a Comment