Monday, September 23, 2013

NAPOLI BADO HAIJAFIKIA KILELE CHAKE - BENITEZ.

MENEJA wa klabu ya Napoli, Rafael Benitez amesisitiza kuwa kikosi chake hakijafikia kiwango chake cha ubora kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AC Milan katika mchezo wa Ligi ya Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A uliofanyika jana. Mabao yaliyofungwa na Miguel Angel Britos na Gonzalo Higuain yaliisaidia Napoli kupata ushindi mwembamba katika Uwanja wa San Siro na kukwea mpaka katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Serie A wakipishana kwa tofati ya mabao na vinara AS Roma. Pamoja na matokeo hayo Benitez anaamini kuwa Napoli bado ina nafasi kucheza vizuri zaidi ya ilivyo sasa na kuahidi kufanyia kazi mapungufu yaliyopo ili waweze kufanya vizuri zaidi huko mbele. Benitez pia aliwasifu wapinzani wao kwa kucheza vyema na kuwapa wakati mgumu mpaka dakika za mwisho huku akimsifu nyota wa Milan Mario Balotelli kwa kuwasumbua mabeki wake muda wote wa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment