Monday, September 23, 2013

GABON YAMTIMUA KOCHA WAKE.

SHIRIKISHO la Soka la Gabon limetangaza kumtimua kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Paulo Duarte kufuatia kuenguliwa katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Katika taarifa yake shirikisho hilo lilidai kufikia hatua baada ya kuona mwenendo mbovu wa timu hiyo ambayo mbali na kushindwa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia lakini ilishindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika iliyofanyika mapema mwaka huu. Taarifa hiyo iliongeza kuwa kocha huyo Mreno hataondoka moja kwa moja kwani ataendelea kufanya kazi kama mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho hilo. Duarte mwenye umri wa miaka 44 pia amewahi kuinoa timu ya taifa ya Burkina Faso 2008 mpaka 2012 kabla hajatimuliwa kwa kushindwa kufanya vyema katika michuano ya mataifa ya Afrika iliyofanyika Gabon na Equatorial Guinea mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment