Monday, September 23, 2013

MOYES ASINGIZIA RATIBA NGUMU.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amelalamikia ratiba ngumu ya waliyopangiwa timu yake msimu huu kufuatia kipigo cha mabao 4-1 walichopata kutoka kwa mahasimu wao Manchester City. Kufuatia kipigo hicho cha jana ambacho kimeiacha United ikigaagaa katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi, Moyes amerudia tena kauli yake kwamba wamepangiwa ratiba ngumu mwanzoni mwa msimu. Moyes amesema ana wasiwasi na ratiba ilivyopangwa kwani anaona kama ilipendelea na kuipa timu yake wakati mgumu mwanzoni. Mwanzoni mwa kampeni yao ya kutetea taji lao la ligi United walipoteza mchezo dhidi ya Liverpool kwa kufungwa bao 1-0 na baadae kutoa sare ya bila kufungana na Chelsea katika Uwanja wa Old Trafford. Lakini pamoja na malalamiko hayo Moyes amepania kusahau matokeo hayo na kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo kwani msimu wa ligi bado mrefu na wana nafasi ya kurejesha morali yao ya ushindi.

No comments:

Post a Comment