MABINGWA wa soka barani Ulaya na Ujerumani, klabu ya Bayern Munich wametangaza kuwa kiungo wake nyota Javi Martinez amefanyiwa upasuaji wa kinena wenye mafanikio. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa hiyo imedai kulikuwa na ulazima wa kiungo wa kimataifa wa Hispania kufanyiwa upasuaji huo baada ya mara kwa mara kulalamika kuwa na tatizo hilo. Martinez ambaye aliingia uwanjani akitokea benchi na kufunga bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi katika muda wa nyongeza wiki iliyopita katika mchezo wa Supercup dhidi ya Chelsea kabla ya Bayern kushinda mechi hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Kocha wa Hispania Vicente del Bosque hakumjumuisha kiungo huyo katika kikosi chake ambacho kinakabiliwa na mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Finland na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Chile.
No comments:
Post a Comment