JEAN Todt, rais wa shirika linaloongoza mchezo wa mbio za langalanga duniani FIA, atakabiliwa na upinzani kwa urais wake mwezi Desemba, baada ya David Ward kutangaza kugombea nafasi hiyo. Ward ambaye ni mkurugenzi mkuu wa shirika huru la hisani la Taasisi ya FIA, amejiuzulu nafasi yake hiyo baada ya miaka 12, ili apambane dhidi ya Todt. Ward mwenye umri wa miaka 56, amesema kipindi cha uchaguzi kinaanza mwezi huu wa Septemba, hivyo ilikuwa muhimu kwake kuwafikia wanachama wa FIA ili aweze kupata uteuzi. Todt alimrithi Max Mosley kama rais wa FIA mwaka 2009, baada ya kumshinda Ari Vatanen katika uchaguzi wa baraza kuu ya FIA, lakini Mfaransa huyo bado hajathibitisha iwapo anataka kugombea muhula wa pili baada ya muhula wake wa sasa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu. Ward anajivunia mtandao mkubwa wa kisiasa ndani ya FIA, unaotokana na nafasi yake ya zamani kama msaidizi wa Mosley.
No comments:
Post a Comment