Monday, September 16, 2013

NEYMAR NI ZAIDI YA RONALDO - WAKALA.

WAKALA wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona, Neymar aitwae Wagner Ribeiro anaamini kuwa nyota huyo yuko katika kiwango cha juu kuliko ilivyokuwa kwa mshambuliaji wa Real Madrid wakati akiwa na umri wa miaka 21. Mwishoni wa wiki iliyopita wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes alidai kuwa hakuna uwezekano kwamba Neymar ni mchezaji mzuri kama ilivyo kwa Ronaldo. Akijibu tuhuma hizo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter Ribeiro amedai kuwa wachezaji hao wawili wote wamezaliwa Februari 5 lakini akasisitiza kuwa Ronaldo hakuwa katika cha juu kama cha Neymar wakati alipokuwa na umri wa kinda huyo. Neymar alijiunga na Barcelona akitokea Santos katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi msimu huu baada ya kuisadia klabu hiyo kushinda Copa Libertadores mwaka 2011 na pia kushinda Kombe la Shirikisho na timu ya taifa ya Brazil Juni mwaka huu. Ronaldo alikuwa na mkataba na klabu ya Manchester United wakati akiwa na umri wa miaka 21 baada ya kuondoka Sporting Lisbon mwaka 2003.

No comments:

Post a Comment