Thursday, September 5, 2013

NINGEPENDA KUINOA LIVERPOOL NIKISTAAFU - GERRARD.

KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Uingereza, Steven Gerrard amesema kwa mara ya kwanza kuwa angependa kuwa meneja wa Liverpool hapo baadae. Gerrard ambaye atakiongoza kikosi cha nchi hiyo kwa ajili ya mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Moldova Ijumaa amekiri kuangalia muda wake uliobakia baada ya kumuona Jamie Carragher akistaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita. Na wakati Carragher akifanya kazi za uandishi katika mtandao wa Sportmail na pia kuwa mchambuzi katika luninga ya Sky Sports, Gerrard yeye anataka kuwa meneja wa Liverpool baada ya kustaafu. Akifanyiwa mahojiano na luninga ya Sky Sports, Gerrard alidai kuwa ndoto zake zitatimia kama ataifundisha Liverpool katika siku za baadae. Gerrard amesema ingawa anajua itakuwa kazi ngumu kutokana na makocha bora kabisa duniani waliopo hivi sasa atasubiri aone wakati wake ukifika itakuwaje. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa ni jambo la kawaida kwa mchezaji yoyote anapofikia umri wake kuangalia kitu cha kufanya baada ya kustaafu.

No comments:

Post a Comment