CHAMA cha soka nchini Misri-EFA bado kinaendelea kutafuta uwanja kwa kuandaa mechi yao ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Guinea Jumanne ijayo. Mapema EFA ilitangaza kuutumia Uwanja wa Borg Al Arab uliopo jijini Alexandria kwa ajili ya mechi hiyo kabla ya Wizara ya mambo ya Ndani kukataa kuwapa usalama katika uwanja huo. Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Misri Diaa Al Sayed amesema kwasasa hawajua watacheza mechi hiyo wapi lakini bodi ya EFA imewaahidi kuwatatulia tatizo hivyo hivyo wanachofanya ni kufanya mazoezi na kusubiri. Msemaji wa EFA Azmy Megahed amebainisha kuwa mazungumzo ya kutaka kutumia Uwanja wa El Defaa El Gawy uliopo jiji Cairo yanaendelea na kuongeza kuwa anadhani Shirikisho la Soka Barani Afrika-CAF litawaelewa kutokana na matatizo yaliyopo. Misri ndio wanaongoza kundi lao wakiwa na alama 15 na tayari wameshafuzu hatua ya mtoano ambayo itashirikisha timu 10 Novemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment