KLABU ya soka ya Simba inatariwa kucheza mechi ya kirafiki kesho na Mabingwa wa Soka wa Ligi Kuu ya Zanzibar, KMKM mchezo ambao utachezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Katika taarifa iliyotumwa na Msemaji wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga imedai kuwa lengo kuu la mechi hiyo ni mazoezi kwa Simba ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa kikosi kamili cha KMKM kimewasili jijini Dar es Salaam tayari na leo saa tano na nusu kamili ambapo nahodha wake, Abdi Kassim Babi na kocha mkuu wa timu hiyo wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika mgahawa wa City Lounge katikati ya jiji. Wakati huohuo Simba inaendelea na mazoezi yake jijini na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya mechi hiyo. Mechi hiyo itaanza majira ya saa 11 jioni ili kuwezesha watu wengi kwenda uwanjani kutazama mechi hiyo ikizingatiwa kuwa Ijumaa ni siku ya kazi.
KATIBA MPYA YA SIMBA
KUFUATIA klabu ya Simba kutaka kuifanyia marekebisho katiba yake kwa Mkutano wa Katiba Novemba mwaka huu, klabu hiyo imeamua kuanzisha mtandao wa barua pepe utakaowawezesha wanachama kutoa mawazo yao juu ya aina ya katiba wanayohitaji. Katika taarifa yake Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema lengo haswa la kufanya hivyo ni kuonyesha umuhimu wa mawazo ya Wana Simba ndani na nje ya nchi. Barua pepe hiyo itajulikana kwa jina la maoniyakatibayasimba@gmail.com ambapo wana Simba na wapenzi wa soka kwa ujumla wanatarajiwa kuwasilisha mawazo na michango yao kuhusu nini kinapaswa kuingizwa katika Katiba mpya ya klabu. Uongozi wa Simba unawaomba wapenzi na washabiki wa soka popote walipo duniani kuchangia mawazo katika njia hii. Mawazo yatakayochangiwa kwenye email hii yatatumika katika kutengeneza rasimu ya Katiba hiyo na rasimu hiyo itapelekwa kwenye matawi yote ya klabu kwa ajili ya kujadiliwa na wanachama. Mawazo hayo ya wanachama yatasaidia katika kutengeneza Katiba ambayo hatimaye itawasilishwa kwenye Mkutano wa Novemba kwa ajili ya mapitio na kupitishwa.

No comments:
Post a Comment