LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya tatu kesho (Septemba 14 mwaka huu) kwa timu zote 14 kushuka viwanjani huku masikio ya washabiki wengi yakielekezwa kwenye mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar na ile kati ya Mbeya City na Yanga. Simba inaikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Dominic Nyamisana kutoka Dodoma. Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Pia Azam TV itautumia mchezo huo kwa ajili ya mazoezi (broadcast training) kwa wafanyakazi wake. Hivyo mechi hiyo haitarekodiwa au kuoneshwa moja kwa moja. Katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, shughuli itakuwa kati ya mabingwa watetezi Yanga na wenyeji wao Mbeya City SC. Mwamuzi Andrew Shamba kutoka Pwani ndiye atakayepuliza filimbi wakati Kamishna wa mechi hiyo James Mhagama kutoka Songea. Mechi nyingine za ligi hiyo ni Coastal Union na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Ruvu Shooting na Mgambo Shooting (Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani), Oljoro JKT na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Kagera Sugar na Azam (Uwanja wa Kaitba, Bukoba), na Ashanti United na JKT Ruvu (Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam).
MJINI MAGHARIBI KUCHEZA FAINALI COPAMjini Magharibi imepata tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 upande wa wavulana baada ya kuing’oa Temeke kwenye nusu fainali iliyochezwa leo (Septemba 13 mwaka huu) asubuhi Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam. Ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa dakika za 30 na 63 kupitia Juma Ali Yusuf ndiyo yaliyoipa Mjini Magharibi tiketi ya kucheza fainali itakayofanyika kesho (Septemba 14 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kuanzia saa 9 alasiri. Mjini Magharibi itacheza fainali hiyo na mshindi wa nusu fainali ya pili inachezwa leo jioni kwenye uwanja huo huo kati ya mabingwa watetezi Morogoro na Ilala. Kwa upande wa wasichana Ilala imetinga fainali baada ya kuifunga Kinondoni mabao 2-0 katika nusu fainali ya kwanza. Mabao ya washindi yalifungwa dakika ya 27 na Fatuma Bahau wakati Happiness Lazoni alifunga la pili dakika ya 39. Nusu fainali ya pili kwa wasichana itakuwa kati ya Mwanza na Mbeya.
30 WAITWA KAMBINI TWIGA STARSKocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage ameita kambini kikosi cha wachezaji 30, wengi wao wakiwa vijana ikiwa ni mwendelezo wa programu ya kujenga timu hiyo. Kambi hiyo itakuwa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 15 hadi 26 mwaka huu. Vijana wengi wamejumuishwa ikiwa ni hatua ya mwanzo ya kuandaa timu itakayocheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20. Kaijage amesema pamoja na malengo hayo kwa timu ya vijana, bado maana kubwa inabaki kuandaa Twiga Stars iliyo imara kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya kimataifa. Amesema Twiga Stars haikabiliwi na mashindano yoyote mwaka huu, hivyo lengo ni kuijenga upya ndiyo maana haichezi michezo ya kimataifa ya kirafiki hadi itakapofika wakati wake. Utaratibu huo ulianza kuanzia kambi ya Machi mwaka huu, na ndio umezaa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ambayo sasa itashiriki mashindano ya Kombe la Dunia. Wachezaji walioitwa ni Amina Ally (Lord Barden, Pwani), Asha Rashid (Mburahati Queens, Dar es Salaam), Belina Julius (Lord Barden, Pwani), Donisia Daniel (Lord Barden, Pwani), Esther Chabruma (Sayari Queens, Dar es Salaam), Eto Mlenzi (JKT, Dar es Salaam) na Evelyn Sekikubo (Mburahati Queens, Dar es Salaam). Fatuma Bushiri (Simba Queens, Dar es Salaam), Fatuma Hassan (Mburahati Queens, Dar es Salaam), Fatuma Issa (Evergreen, Dar es Salaam), Fatuma Mustafa (Sayari Queens, Dar es Salaam), Fatuma Omari (Sayari Queens, Dar es Salaam), Flora Kayanda (Tanzanite, Dar es Salaam) na Gerwa Lugomba (Umisseta, Kanda ya Ziwa). Hamisa Athuman (Marsh Academy, Mwanza), Maimuna Hamisi (Airtel Rising Star, Ilala), Maimuna Said (JKT, Dar es Salaam), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens, Dar es Salaam), Mwapewa Mtumwa (Sayari Queens, Dar es Salaam), Pulkeria Charaji (Sayari Queens, Dar es Salaam) na Rehema Abdul (Lord Barden, Pwani). Sabahi Hashim (Umisseta, Zanzibar), Semeni Abeid (Tanzanite, Dar es Salaam), Sharida Boniface (Makongo Sekondari, Dar es Salaam), Sofia Mwasikili (Sayari Queens, Dar es Salaam), Tatu Idd (Lord Barden, Pwani), Therese Yona (TSC Academy, Mwanza), Vumilia Maarifa (Evergreen, Dar es Salaam), Yulitha Kimbuya (Marsh Academy, Mwanza) na Zena Khamis (Mburahati Queens, Dar es Salaam).

No comments:
Post a Comment