RAIS wa klabu ya Bayern Munich, Uli Hoeness anaamini kuwa klabu hiyo haikukosea kumuacha kocha wa zamani Jupp Heynckes na nafasi yake kuchukua Pep Guardiola. Bayern walimuacha kocha huyo wa zamani ambaye alifanikisha timu hiyo kuweka historia kwa kushinda mataji matatu msimu uliopita baada ya kuwa tayari wameshakubaliana kumpa mkataba Guardiola. Guardiola amekuwa akipondwa na baadhi ya mashabiki wakihoji uwezo wake wa kufundisha lakini Hoeness alimtetea na kudai kuwa hakuna haja ya kumfananisha na Heynckes kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanarudisha soka lao nyuma. Hoeness amesema Heynckes alimhakikishia kuwa muda wake wa kuachana kazi ya ukocha ulikuwa umefika hivyo binafsi anadhani walifanya chaguo sahihi kumchukua Guardiola kuchukua kibarua hicho.

No comments:
Post a Comment