JIJI la Tokyo kupewa uenyeji wa kuandaa michuano ya olimpiki 2020 kunamaanisha kuwa Ujerumani inatarajia kukosa nafasi ya kuandaa fainali ya michuano ya soka ya Ulaya 2020. Tokyo ilipatiwa nafasi ya kuandaa michuano hiyo na kamati ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC jijini Buenos Aires, Argentina baada ya kuwashinda wapinzani wao miji ya Istanbul na Madrid. Mapema Shirikisho la Soka nchini Ujerumani-DFB lilidai kuwa litajiondoa katika kinyang’anyiro cha kuandaa fainali ya michuano ya Ulaya dhidi Istanbul kama mji huo mkuu wa Uturuki hautapata nafasi ya kuandaa michuano ya olimpiki. DFB tayari ilikuwa imeshateua Uwanja wa Allianz Arena uliopo jijini Munich kuwa uwanja utakaoshindaniwa katika kinyang’anyiro hicho wakati Shirikisho la Soka barani Ulaya likijipanga kutangaza miji 13 itakayopewa uenyeji Septemba mwakani. Kwa mara ya kwanza michuano ya Ulaya 2020 inatarajiwa kufanyika katika miji mbalimbali kuzunguka bara ya Ulaya na sio nchi moja kama ilivyozoeleka.
No comments:
Post a Comment