Tuesday, September 24, 2013

VAN PERSIE KUIKOSA LIVERPOOL.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester United anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwenye mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool baadae leo. Nyota huyo alipata majeraha ya msuli kabla ya mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester City uliofanyika katika Uwanja wa Etihad Jumapili iliyopita. Akihojiwa kuhusiana na hali ya Van Persie, meneja wa United David Moyes alithibitisha kumkosa nyota huyo katika mchezo dhidi ya Liverpool lakini anategemea atakuwa fiti kwa ajili ya mechi dhidi ya West Brom JUmamosi ijayo. Moyes pia amesema huu ni wakati wa kusahau kipigo cha mabao 4-1 walichopata kutoka kwa mahasimu wao City na anaamini bado anaendelea kuwaelewa wachezaji wake vyema.

No comments:

Post a Comment