Tuesday, September 24, 2013

BALE KUIVAA ATLETICO - ANCELOTTI.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid amethibitisha kuwa mshambuliaji wake nyota Gareth Bale atakuwa fiti kabla ya mchezo dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid utakaopigwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu Jumamosi. Bale alitakiwa kuwepo katika kikosi cha Madrid kilichoisambaratisha Getafe kwa kushinda mabao 4-1 Jumapili iliyopita lakini ilishindikana baada ya kuumia dakika za mwisho kabla ya kuanza kwa mechi hiyo. Ancelotti amesema nyota tayari ameanza kuafanya mazoezi mepesi mwenyewe na anadhani mpaka Jumamosi atakuwa tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Atletico. Kocha pia alikanusha tuhuma kwamba amewahi kumtumia mchezaji huyo mapema baada ya kujiunga na Madrid akitokea klabu ya Tottenham Hotspurs kwa uhamisho uliovunja rekodi.

No comments:

Post a Comment