VILABU vikubwa barani Ulaya vimedai kuwa vipo tayari kuangalia uwezekano wa michuano ya Kombe la Dunia kuchezwa katika majira ya baridi nchini Qatar 2022. Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter ametaka michuano hiyo kuhamishwa kwasababu ya wasiwasi wa jinsi gani wachezaji wanaweza kupambana na hali ta joto kali ambalo hufikia nyuzi joto 40 katika kipindi cha majira ya kiangazi. Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu vya Ulaya, Karl-Heinz Rummenigge ambaye anawakilisha vilabu vikubwa amesema labda itakuwa vyema kucheza michuano hiyo katika majira ya baridi na kuongeza kuwa hawana haraka ya kufanya maamuzi kwasababu bado kuna miaka tisa mbele. Toka Qatar iliposhinda haki za kuandaa michuano hiyo mwaka 2010, suala la michuano hiyo kufanyika katika kipindi cha majira ya kiangazi katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati limekuwa likizua mjadala mkubwa. Hata hivyo Ofisa Mkuu wa Ligi Kuu nchini Uingereza Richard Scudamore ameonyesha kupingana na kauli ya Rummenigge akidai kuwa michuano hiyo inaweza kufanyika katika majira ya kiangazi pekee. Uingereza ina timu 10 katika chama hicho ambzo ni Arsenal. Aston Villa, Everton, Fulham, Liverpool, Manchester City, Manchester United, Newcastle United na Tottenham Hotspurs.
No comments:
Post a Comment