BONDIA Darren Barker wa Uingereza anatarajiwa kupigana kwa mara ya kwanza kutetea taji lake la IBF uzito wa kati dhidi ya Felix Sturm wa Ujerumani Desemba 7 mwaka huu. Barker mwenye umri wa miaka 31 alishinda taji hilo kwa alama dhidi ya Daniel Geale wa Australia katika pambano lilifanyika Atlantic City Agosti mwaka huu. Akihojiwa kuhusiana na pambano hilo promota wa Barker aitwaye Eddie Hearn amesema kuna makubaliano ya kuwepo pambano la marudiano jijini London kama bondia wake akitandikwa katika pambano hilo. Sturm ambaye alidundwa na Geale Septemba mwaka jana ana rekodi ya kushinda mapambano 38 ambapo 17 kati ya hayo alishinda kwa knockout, kupigwa matatu na sare mapambano mawili. Kwa upande wa Barker yeye ameshinda mapambano 26 kati ya 27 akiwa chini promota wake Hearn.
No comments:
Post a Comment