WARATIBU wa michuano ya wazi ya Australia wameongeza zawadi kwa washindi wa michuano hiyo kwa asilimia 10 mpaka kufikia dola milioni 33 kwa mwaka 2014. Mwaka jana zawadi za jumla katika michuano hiyo zilifikia dola milioni 30 ambapo bingwa kwa upande wa wanaume Novak Djokovic na wanawake Victoria Azarenka kila mmoja alipokea hundi ya dola milioni 2.43. Hatua ya kuongeza zawadi katika michuano hiyo mikubwa kabisa ambayo hufanyika jijini Melbourne Januari ya kila mwaka ilifikiwa baada ya baadhi ya wachezaji kulaumu mgao kiduchu kulingana na hadhi yake. Mkurugenzi wa michuano hiyo Craig Tiley amesema wachezaji wameshataarifiwa kuhusiana na mabadiliko hayo na wote wameonyesha kukubaliana nao.
No comments:
Post a Comment