MWANARIADHA nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica, Usain Bolt anatarajiwa kushiriki mbio za mita 100 za maonyesho zitakazofanyika jijini Buenos Aires, Argentina Desemba mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya nchi hiyo Bolt ambaye anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100, atashiriki katika mbio zitakazofanyika Desemba 7 au 13. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo mratibu wa mbio hizo za hisani, Guillermo Marin alithibitisha ujio wa Bolt na kudai kuwa nyota huyo atakuja na wanariadha wengine watatu kutoka Jamaica. Marin pia amesema mbali na kufanyika kwa mbio hizo kutakuwa na mchezo wa tenisi wa hisani ambao utawahusisha wanadada wawili ndugu kutoka Marekani Venus na Serena Williams.
No comments:
Post a Comment