Wednesday, October 2, 2013

TORRES KUFANYIWA UCHUNGUZI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Chelsea, Fernando Torres anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa mguu wake ambao aliumia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Steaua Bucherest iliyochezwa jana. Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho amesema kuwa mchezaji huyo hatakuwa fiti kwa ajili ya kwenda kuitumikia timu ya taifa ya Hispania wiki ijayo lakini ana matumaini tatizo lililompata sio kubwa sana. Mourinho aliendelea kudai kuwa madaktari wa timu hiyo wana uhakika majeruhi aliyopata sio makubwa sana kama aliyopata Marco van Ginkel ya kukaa nje ya uwanja miezi sita. Torres mwenye umri wa miaka 29 tayari hayumo katika kikosi cha timu hiyo kitakachopambana na Norwich City Jumapili kufuatia kutolewa nje kwa kadi mbili za njano kwenye mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment