Friday, October 18, 2013

BAYERN KUMPA LEWANDOWSKI PAUNDI MILIONI 10 KWA MWAKA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Borussia Dortmund Robert Lewandowski atakunja kitita cha paundi milioni 10 wakati atakapojiunga na Bayern Munich kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu huu. Mabosi wa Bayern wamepuuza taarifa kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Poland ameamua kubadili mawazo kujiunga na klabu hiyo na kusisitiza kuwa uvumi huo utakwisha wakati watakapofanya usajili wa awali katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Katika kipindi hiki haruhusiwi kufanya mazungumzo yoyote rasmi kuhusiana na uhamisho huo mpaka Januari lakini kumekuwa na tetesi kuwa Bayern wamepanga kumpa mkataba mnono wa miaka minne ambao utamuwezesha kuwa analipwa kiasi cha paundi 150,000 kwa wiki. Taarifa zozote rasmi za Bayern kumnyakuwa nyota huyo zitakuwa ni pigo kwa vilabu vya Manchester United na Chelsea ambao nao wamekuwa wakimtolea macho kwa kutaka kumsajili.

No comments:

Post a Comment