Friday, October 18, 2013

LOEW AONGEZA MKATABA NA UJERUMANI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amefikia makubaliano na Chama cha Soka cha nchi hiyo-DFB juu ya mkataba mpya ambao utamalizika mwaka 2016. Mkataba wa sasa wa Loew mwenye umri wa miaka 53 ulikuwa unamalizika baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 lakini sasa amemaliza tetesi juu ya mustakabali wake kwa kusaini mkataba huo wa miaka miwili. Loew alichukua mikoba ya kuinoa Ujerumani mwaka 2006 baada ya kufanya kazi kama msaidizi wa Jurgen Klinsmann katika timu hiyo. Kocha huyo ameiongoza Ujerumani kutinga fainali ya michuano ya Ulaya 2008 ambapo walifungwa na Hispania kwa bao 1-0 kabla ya kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2010 na ile ya Ulaya 2012.

No comments:

Post a Comment