Tuesday, October 22, 2013

BRUNO METSU AZIKWA KWA HESHIMA ZOTE SENEGAL.

KOCHA wa zamani wa Senegal Bruno Metsu,ambaye alifariki Jumanne wiki iliyopita huko Ufaransa, amezikwa jana jijini Dakar, Senegal, mazishi yaliyohudhuriwa na watu mbalimbali na akizikwa kwa heshima kubwa. Metsu alibadili dini na kuwa Muislam wakati alipokuwa akiwafundisha Simba wa Teranga Senegal kati ya mwaka 2000 na 2002 na akaoa mwanamke wa Senegal Viviane Dieye, ambaye amesema kocha huyo alitaka azikwe Dakar. Jeneza lake lilifunikwa na bendera ya nchi hiyo aliyoiongoza kwenye fainali za dunia za mwaka 2002 na amezikwa kwenye makaburi ya waislam ya Yoff. Metsu anaelezewa kama shujaa wa nchi hiyo ambaye moyo wake ulikuwa na mapenzi halisi na nchi hiyo. Kocha huyo kwa mara ya mwisho amefanya kazi ya ukocha huko Dubai kwenye klabu ya Al Wasl FC mwaka 2012 kabla ya kuiacha kazi hiyo na kwenda kupata matibabu ya kansa ya ini na mapafu huko Ufaransa. Amefariki kwenye sehemu alikozaliwa kijiji cha Coudekerque Kaskazini mwa Ufaransa na akasafirishwa kwa maziko yaliyofanyika hiyo jana nchini Senegal.

No comments:

Post a Comment