Tuesday, October 22, 2013

FA KUMCHUKULIA HATUA MOURINHO.

CHAMA cha Soka Cha Uingereza-FA kimemshitaki meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho kwa tabia isiyo ya kiungwana aliyoionyesha katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Cardiff City mwishoni mwa wiki iliyopita. Mourinho aliamriwa kwenda kukaa jukwaani na mashabiki na mwamuzi Anthony Taylor zikiwa zimebaki dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika baada ya kulalamika mara kwa mara kwamba Cardiff walikuwa wakipoteza muda. Kocha huyo ambaye amepewa mpaka Alhamisi kujibu tuhuma hizo, alikataa kuomba radhi kuhusiana na tukio hilo wakati akihojiwa kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Schalke ya Ujerumani. Mourinho amesema Cardiff ambao walifungwa mabao 4-1 katika mchezo huo walikuwa wakipoteza muda kila wakati ambao mwamuzi anakuwa amepuliza filimbi aidha kwa ajili ya faulo au mpira wa kurusha. Mourinho aliendelea kudai kuwa mashabiki wanalipia tiketi zao kwa ajili ya kutazama burudani ya soka na sio timu moja ipoteze muda ili mchezo umalizike haraka.

No comments:

Post a Comment