KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya Stade Malien katika mchezo uliofanyika jijini Bamako, Mali. Nyota wa Mazembe Rainford Kalaba na Tresor Mputu wote kwa pamoja waliifungia timu hiyo katika ushindi wa mabao 2-1 iliyopata huku bao la wenyeji likifungwa na Morikaman Koita. Nia ya Mazembe ilikuwa ni kupata matokeo mazuri ugenini huku wakitegemea kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa nyumbani wakati watakapokwaana kaika mechi ya mkondo wa pili itakayofanyika jijini Lubumbash. Mshindi wa jumla kati ya timu hizo atakwaana na mojawapo ya timu za Bezertin na Sfaxien zote za Tunisia katika fainali ambayo itachezwa kwa mikondo miwili.
No comments:
Post a Comment