Monday, October 7, 2013

DEL BOSQUE AMUITA MICHU KUZIBA NAFASI YA VILLA, HISPANIA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amemuita mshambuliaji wa Swansea City Michu katika kikosi chake ili kuziba nafasi ya majeruhi David Villa katika mechi mbili za mwisho za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Belarus na Georgia. Villa ambaye anakipiga katika klabu ya Atletico Madrid aliondelewa katika kikosi cha Hispania baada ya kuumia kifundo chake cha mguu wa kushoto. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa Atletico ilithibitisha taarifa hizo baada ya daktari wake timu Juan Cota kumfanyia vipimo nyota huyo ili kugundua ukubwa wa tatizo. Michu mwenye umri wa miaka 27 ambaye amekuwa aking’ara katika Ligi Kuu nchini Uingereza toka atue Swansea akitokea Rayo Vallecano hajawahi kuichezea timu yake ya taifa. Hispani inatarajia kucheza na Belarus Octoba 11 jijini Mallorca na mechi nyingine dhidi ya Georgia siku nne baadae.

No comments:

Post a Comment