MCHEZA tenisi mahiri Juan Martin del Porto amefanikiwa kushinda michuano ya wazi ya Japan baada ya kumgaragaza Milos Raonic wa Canada. Del Porto mwenye umri wa miaka 25 alifanikiwa kushinda taji hilo kwa kumfunga Rionic seti 2-0 zenye alama za 7-6 7-5. Nyota huyo wa tenisi kutoka Argentina alipata nafasi ya kushiriki michuano hiyo baada ya Andy Murray wa Uingereza kujitoa kutokana na majeraha. Hilo linakuwa taji la tatu mwaka huu kwa Del Porto ambaye aliwahi kushinda michuano ya wazi ya Marekani mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment