KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vecente del Bosque amekiri kuwa timu yake ilipata tabu kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Belarus jana na ameonyesha wasiwasi wake wa kiwango kilichoonyeshwa na kikosi chake kwenye mchezo huo. Iliwachukua saa moja kwa Hispania kufanikiwa kuliona lango la wapinzani wao katika mchezo huo uliochezwa jijini Mallorca bao lililofungwa na Xavi kabla ya Alvaro Negredo kuongeza lingine muda mfupi baadae. Pamoja na ushindi huo Del Bosque ameonyesha kutofurahishwa na kikosi chake kushindwa kucheza kwa kiwango chao kilichozoeleka katika mechi za karibuni. Kocha huyo amesema ni ukweli usiopingika kwamba ushindi huo umekuwa tabu kwao baada ya kushindwa kufunga bao mpaka dakika 15 ya kipindi cha pili na imewatokea hivyo katika mechi kadhaa walizocheza karibuni. Del Bosque amesema pamoja na hayo kitu cha muhimu wamepiga hatua kwa ajili ya kufuzu Kombe la Dunia na makosa yalitokea watayafanyika kazi ili mechi inayofuata mambo yaweze kuwa mazuri zaidi.
No comments:
Post a Comment