IKIWA imebaki hatua moja kufikia michuano ya Kombe la Dunia baada ya mechi za kufuzu zilizochezwa jana duniani kote, mataifa manne zaidi tayari yameshajihakikishia nafasi ya kushiriki michuano hiyo itakayofanyika Brazil mwakani. Wenyeji wa michuano hiyo tayari wameshaungana na wawakilishi kutoka bara ya Asia ambao ni Japan, Australia, Iran na Korea Kusini katika hatua za mapema, pamoja na Uholanzi na Italia kwa upande wa Ulaya, Argentina kwa upande wa Conmebol huku Costa Rica na Marekani wao wakiwakilisha nchi za Concacaf. Katika mechi za jana nchi nyingine kutoka bara la Ulaya na Amerika Kusini ziliongezeka katika orodha hiyo ambapo kwa upande wa Ulaya nchi za Ubelgiji, Ujerumani na Switzerland zilijihakikishia nafasi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kushinda mechi zao. Kwa upande wa Amerika Kusini Colombia nao walijikatia teketi ya moja kwa moja baada ya kufanikiwa kuifunga Chile na kuungana na miamba mingine ya upande huo kama Argentina na Brazil.
No comments:
Post a Comment