KLABU ya Internacional ya Brazil imemtimua kocha wake Dunga baada ya kupata kipigo cha nne mfululizo katika Ligi Kuu ya nchi hiyo. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo ilidai kulibadilisha benchi zima la ufundi la klabu hiyo akiwemo kocha mkuu. Klabu hiyo imemteua kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 20 aitwae Clemer kushikilia nafasi hiyo kwa muda wa mchakata wa kutafuta kocha mwingine ukiendelea. Dunga ambaye aliiwezesha timu hiyo kushinda mechi 26 na kupoteza tisa katika mechi 53 ambazo imecheza, alitimuliwa wakati wakiwa Rio de Janeiro ambapo walichapwa mabao 3-1 na Vasco da Gama.
No comments:
Post a Comment