MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo anatarajia kukata rufani kwa maofisa wa jiji la Florida ili kufuta kesi ya shabiki aliyekamatwa kwa kosa la kuvamia uwanja na kwenda kumkumbatia nyota huyo. Ronaldo ambaye ni mwanasoka anaelipwa zaidi duniani alilichukulia tukio hilo lililofanyika Agosti mwaka huu kirahisi na hata kufikia hatua ya kuzungumza na shabiki huyo mwenye miaka 19 na kuwaomba polisi wasimpige wakati wakimtoa uwanjani. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno sasa anataka kuwaomba waendesha mashitaka kumuachia shabiki huyo ambaye ni mwanafunzi kutoka Canada ambaye anashitakiwa kwa makosa mawili aliyofanya wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Madrid na Chelsea. Shabiki huyo Ronald Gjoka alilala lupango kwa siku moja baada ya kufanya tukio hilo mbele ya mashabiki wapatao 70,000 waliohudhuria mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment