Sunday, October 6, 2013

KLITSCHKO ATETEA MATAJI YAKE.

MBABE wa masumbwi Wladimir Klitschko amefanikiwa kutetea mataji yake ya uzito wa juu duniani ya WBA, IBF na WBO baada ya kumtandika Alexander Povetkin wa Urusi.  Katika pambano hilo Povetkin ambaye hakuwahi kupigwa kabla ya pambano hilo, aliangushwa mara tatu katika raundi ya saba na alionekana hana madhara mbele ya Klitschko. Majaji wote watatu walikuwa wakifuatilia pambano hilo kwa karibu walitoa alama 119 kwa Klitschko huku mpinzani wake akipewa alama 104. Klitschko ambaye ni raia wa Ukraine amefanikiwa kushinda mapambano 15 ya kutetea mataji yake na kujiwekea rekodi ya kushinda mapambano 61 kati 64 aliyopigana kattika ngumi za kulipwa.

No comments:

Post a Comment