MSHAMBULIAJI kinda mzaliwa wa Ubelgiji, Adnan Januzaj ameombwa kuichezea timu ya taifa ya Uingereza inayonolewa na Roy Hodgson wakati Manchester United wakijipanga kumpa mkataba wa muda mrefu kinda huyo. Meneja wa United, David Moyes alibainisha kuwa Chama cha Soka cha Uingereza tayari kimefuata kinda huyo kuhusu kuichezea nchi hiyo. Nyota huyo alicheza dakika zote katika mchezo wa jana na kufunga mabao mawili muhimu ambayo yalipelekea United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sunderland. Mbali na kuwa mzaliwa wa Ubelgiji Januzaj pia ana uwezo wa kucheza katika timu za taifa za Albania na Uturuki.
No comments:
Post a Comment