MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto’o anatarajia kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kilichopo Ufaransa baada ya kubadili uamuzi wake wa kustaafu soka la kimataifa. Eto’o ambaye pia ni nahodha wa Cameroon anatarajia kujiunga na kikosi hicho kinachofanya maandalizi yake jijini Lisses kabla ya mechi yao ya mkondo wa kwanza ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani dhidi ya Tunisia. Hatua ya nyota huyo kubadili uamuzi wake imekuja kufuatia kufanya mazungumzo ya faragha na Katibu Mkuu katika ofisi ya rais ya nchi hiyo, Ferdinand Ngoh ambaye alimpokea kwa niaba ya rais Paul Biya. Mara baada ya mazungumzo hayo Eto’o aliamua kubadili uamuzi wake wa kustaafu na kuahidi kuisadia timu hiyo kufuzu michuano hiyo ya mwakani. Eto’o aliwaambia wachezaji wenzake kwamba anastaafu soka la kimataifa kwa sababu za kifamilia baada ya mechi ya mwisho ya kufuzu hatua ya makundi dhidi ya Libya mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment