Wednesday, October 9, 2013

UTOVU WA NIDHAMU WAMPONZA INCE.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kimemfungia meneja wa klabu ya Blackpool Paul Ince mechi tano kutokana na tabia za utovu wa nidhamu. Ince mwenye umri wa miaka 45 ambaye amewahi kucheza katika klabu za Inter Milan na Manchester United aliingia matatani baada ya kukutwa na kosa la kumshambuliaji mwamuzi wakati wa mechi za Ligi Daraja Kwanza mapema msimu huu. Nyota huyo za zamani ambaye alikuwa akicheza nafasi ya kiungo alishitakiwa kwa kutumia lugha chafu ambapo ambali na adahabu hiyo lakini pia alitozwa faini ya paundi 4,000. Adhabu ambayo inaanza mara moja itamzuia Ince ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza kutohudhuria mechi za ligi kuanzia Octoba 19 mpaka Novemba 30.

No comments:

Post a Comment