RAIS wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell ana uhakika kuwa kiungo mahiri Andres Iniesta atastaafu soka akiwa na timu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa akifanya mazungumzo ya kuongeza mkataba wake kwa wiki kadhaa lakini bado hawajafikia makubaliano na mabingwa hao wa soka wa Hispania. Lakini Rosell haonyeshi kushtushwa na kuchelewa kusainiwa mkataba mwingine akidai kuwa wakati ukifika nyota huyo atasaini mkataba mpya. Rosell amesema Iniesta atamaliza soka lake akiwa Barcelona na anaamini anatakiwa kuwa mchezaji wa pili anayelipwa zaidi katika timu hiyo baada ya Lionel Messi.
No comments:
Post a Comment