Friday, October 11, 2013

FIFA YAMFUNGIA ABOURAZZOUK WA MOROCCO BAADA YA KUKUTWA MAETUMIA MADAWA KATIKA MCHEZO DHIDI YA TANZANIA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limemfungia miezi sita mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco Hamza Abourazzouk baada ya kukutwa na chembechembe za dawa za kusisimua misuli katika damu yake. Abourazzouk mwenye umri wa miaka 27 alikutwa ametumia dawa hizo katika vipimo aivyofanyiwa baada ya mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania Juni 8 mwaka huu. Hata hivyo Morocco walishindwa kufuzu katika michuano hiyo. Nyota huyo anayecheza katika klabu ya Raja Casablanca atakosa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia Desemba mwaka huu ambayo Morocco itakuwa mwenyeji ambapo Raja Casablanca wamefuzu kushiriki michuano hiyo kama mabingwa wa ligi wan chi hiyo.

No comments:

Post a Comment