SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limebainisha kuwa kampuni ya GoalControl ya Ujerumani ndio itakayofunga kamera za mfumo wa teknologia ya kompyuta katika goli katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil na Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia itakayofanyika nchini Morocco mwaka huu. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wake FIFA imedai kuwa mfumo huo ulifanyiwa majaribio katika michuano ya Kombe la Shirikisho mapema mwaka huu baada ya kampuni hiyo kushinda zabuni. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika majaribio ya mfumo huo kwenye Kombe la Shirikisho FIFA inathibitisha kuwa GoalControl ndio watapewa jukumu ya kufunga vyombo vinavyotumia mfumo huo kwenye michuano hiyo. Mfumo wa GoalControl unatumia kamera 14 zenye uwezo wa hali ya juu zinafungwa pembezoni kwa milingoti ya goli ili kuhakiki kama mpira umevuka mstari au la.
No comments:
Post a Comment