Friday, October 11, 2013

DEREVA WA LANGALANGA AKUTWA AMEKUFA HOTELINI.

DEREVA mahiri wa mashindano ya langalanga, Maria De Villota amekutwa amekufa katika chumba cha hoteli aliyofiki jijini Seville Hispania. Mpaka sasa hakuna taarifa zozote zinazoelezea sababu ya kifo cha mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye alipoteza jicho lake la kulia katika ajali wakati akifanya majaribio ya gari la timu ya Marussia mwaka jana. De Villota ambaye ni binti wa dereva wa zamani wa langalanga Emilio De Villota alipata majeraha sehemu mbalimbali za kichwa baada ya kugongana na lori. Mwanadada huyo anadaiwa alikuwepo jijini Seville kwa ajili ya kutambulisha kitabu cha wasifu wake. Timu pamoja na madereva wa langalanga wote wametuma salamu zao za rambirambi kwa kuguswa na msiba huo wa kustusha.

No comments:

Post a Comment