Monday, October 21, 2013

HODGSON, FERDINAND WATEULIWA TUME YA KUCHUNGUZA MATOKEO MABOVU YA UINGEREZA.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kimewateua kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Roy Hodgson na beki wa klabu ya Manchester United Rio Ferdinand kuingia katika tume ya kuchunguza mapungufu ya timu ya taifa. Tume hiyo ambayo itakuwa na watu 10, itakuwa na jukumu la kuangalia njia za kuongeza wachezaji wa Uingereza katika Ligi Kuu ya nchi hiyo na wanatarajiwa kuwasilisha ripoti yao mwishoni mwa Machi mwakani. Kuteuliwa kwa Ferdinand ambaye ni mweusi kumekuja kufuatia mjumbe wa bodi ya FA Heather Rabbatts kumponda mwenyekiti wake Greg Dyke kwa kuchagua wanaume na watu weupe pekee katika tume hiyo. Dyke amesema uteuzi wa Ferdinand umetokana na uzoefu wake katika mchezo wa soka toka alipoanza wakati akiwa West Ham United na kuja kushinda taji la Ligi Kuu naLigi ya Mabingwa barani Ulaya akiwa na United huku akiiwakilisha Uingereza katika michuano kadha ya Kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment