Monday, October 21, 2013

NI MAPEMA KUIONDOA UNITED KATIKA MBIO ZA UBINGWA - WENGER.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene amekataa kuiondoa klabu ya Manchester United katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza pamoja na mabingwa hao watetezi kuwa nyuma Arsenal wanaoongoza ligi hiyo kwa alama nane. Arsenal waliongeza pengo dhidi ya United wanaonolewa na David Moyes Jumamosi baada ya kuifunga Norwich kwa mabao 4-1 wakati United wao walipoteza alama kwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton. Hata hivyo Wenger amesisitiza kuwa mbio za ubingwa haziwezi kuamuliwa sasa hivyo huwezi kuwaondoa United na kuonya kuwa hata wao wanaweza kuporomoka. Wenger amesema hakuna timu inayotaka kuwa katika nafasi ya United hivi sasa lakini anaamini kutokana na uzoefu na ubora wa wachezaji walionao wanaweza kukwea na kupanda huko mbele.

No comments:

Post a Comment