Monday, October 21, 2013

KLOPP ATAMBA KUICHAPA ARSENAL.

MENEJA wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amesema ana uhakika wa ushindi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Arsenal itakayofanyika katika Uwanja wa Emirates. Dortmund watakwenda jijini London wakiwa nyuma ya Arsenal kwa alama tatu kutokana na kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa mabao 2-1 dhidi ya Napoli ya Italia kabla ya kuzinduka na kuibamiza Olympique Marseille ya Ufaransa kwa mabao 3-0. Akihojiwa mara baada ya mchezo wa Bundesliga ambao Dortmund ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Hannover, Klopp amesema ana uhakika wa kufanya vyema katika mechi yao hiyo itakayochezwa kesho. Klopp amesema anajua kwamba Arsenal wako katika kiwango cha juu hivi sasa na wanaongoza ligi lakini hilo haliwezi kuwatisha kasababu anaamini vijana wake wanaouwezo wa kukabiliana na timu yoyote.

No comments:

Post a Comment