KOCHA wa timu ya taifa ya Croatia, Igor Stimac ameamua kujiuzulu baada ya timu yake kupoteza mchezo wake wa mwisho wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa kufungwa mabao 2-0 na Scotland. Croatia imeambulia alama moja pekee katika mechi za nne za kundi A na kuwaacha katika nafasi ya pili kwenye msimamo nyuma ya Ubelgiji huku wakikabiliwa na kibarua cha kucheza mechi za mtoano za mikondo miwili kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kwenda Brazil mwakani. Stimac alichukua mikondo ya kuinoa nchi hiyo mwaka jana akichukua mikoba ya Slaven Bilic. Akihojiwa na Sky Sport mara baada ya mechi hiyo Stimac alisikitishwa na kipigo hicho na kuomba kujiuzulu kwasababu ya matokeo mabovu ambayo kikosi chake imepata katika mechi a karibuni.
No comments:
Post a Comment