Tuesday, October 1, 2013

LENNON MENO NJE.

MENEJA wa klabu ya Celtic ya Scotland, Neil Lennon ameonyesha kutofurahishwa sana na kukosekana kwa Lionel Messi katika kikosi cha Barcelona ambacho watacheza nacho baadae jijini Glasgow. Messi ambaye anashikilia taji la mchezaji bora wa dunia atakosa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kundi H kutokana na majeruhi ya msuli yanayomsumbua. Akihojiwa kuhusiana na mechi hiyo Lennon amesema kwa maoni yake kukosekana kwa Messi ni habari njema kwao lakini kwa upande mwingine inasikitisha kwasababu huwa ni vyema kuwaona wachezaji bora wa dunia wakicheza jijini Glasgow. Messi alikuwepo katika kikosi cha Barcelona kilichofungwa katika Uwanja wa Celtic Park katika hatua ya makundi msimu uliopita lakini hii itakuwa ni mara ya kwanza Neymar kucheza dhidi ya mabigwa hao wa Scotland.

No comments:

Post a Comment