Tuesday, October 1, 2013

DERBY COUNTY YAMNASA MACCLAREN.

KLABU ya Derby County imemtaja kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Steve McClaren kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miaka miwili. McClaren anachukua mikoba ya Nigel Clough ambaye alitimuliwa Jumamosi iliyopita baada ya timu hiyo kupata kipigo kutoka kwa Nottingham Forest. Akihojiwa kuhusiana na hilo ofisa mkuu wa Derby Sam Rush amesema walifikia uamuzi wa kumpa kibarua McClaren kutokana na uzoefu wake na wana imani kuwa atawapeleka mbali. Hata hivyo pamoja na uteuzi huo MacClaren kwenye miaka 52 hatakuwepo katika benchi la ufundi katika mchezo dhidi ya mahasimu wao Ipswich utakaochezwa leo badala yake atakuwepo meneja wa muda Darren Wassall.

No comments:

Post a Comment